Swahili
Surah Al-A'la ( The Most High ) - Aya count 19
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى
( 1 ) Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa,
الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ
( 2 ) Aliye umba, na akaweka sawa,
وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ
( 3 ) Na ambaye amekadiria na akaongoa,
وَالَّذِي أَخْرَجَ الْمَرْعَىٰ
( 4 ) Na aliye otesha malisho,
فَجَعَلَهُ غُثَاءً أَحْوَىٰ
( 5 ) Kisha akayafanya makavu, meusi.
سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰ
( 6 ) Tutakusomesha wala hutasahau,
إِلَّا مَا شَاءَ اللَّهُ ۚ إِنَّهُ يَعْلَمُ الْجَهْرَ وَمَا يَخْفَىٰ
( 7 ) Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana.
وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَىٰ
( 8 ) Na tutakusahilishia yawe mepesi.
فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ الذِّكْرَىٰ
( 9 ) Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa.
سَيَذَّكَّرُ مَن يَخْشَىٰ
( 10 ) Atakumbuka mwenye kuogopa.
وَيَتَجَنَّبُهَا الْأَشْقَى
( 11 ) Na atajitenga mbali nayo mpotovu,
الَّذِي يَصْلَى النَّارَ الْكُبْرَىٰ
( 12 ) Ambaye atauingia Moto mkubwa.
ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ
( 13 ) Tena humo hatakufa wala hawi hai.
قَدْ أَفْلَحَ مَن تَزَكَّىٰ
( 14 ) Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa.
وَذَكَرَ اسْمَ رَبِّهِ فَصَلَّىٰ
( 15 ) Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali.
بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا
( 16 ) Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia!
وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ
( 17 ) Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.
إِنَّ هَٰذَا لَفِي الصُّحُفِ الْأُولَىٰ
( 18 ) Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo,
صُحُفِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ
( 19 ) Vitabu vya Ibrahimu na Musa.