Swahili
Surah Ar-Rahman ( The Most Graciouse ) - Aya count 78
الرَّحْمَٰنُ
( 1 ) Arrah'man, Mwingi wa Rehema
عَلَّمَ الْقُرْآنَ
( 2 ) Amefundisha Qur'ani.
خَلَقَ الْإِنسَانَ
( 3 ) Amemuumba mwanaadamu,
عَلَّمَهُ الْبَيَانَ
( 4 ) Akamfundisha kubaini.
الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ بِحُسْبَانٍ
( 5 ) Jua na mwezi huenda kwa hisabu.
وَالنَّجْمُ وَالشَّجَرُ يَسْجُدَانِ
( 6 ) Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea.
وَالسَّمَاءَ رَفَعَهَا وَوَضَعَ الْمِيزَانَ
( 7 ) Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani,
أَلَّا تَطْغَوْا فِي الْمِيزَانِ
( 8 ) Ili msidhulumu katika mizani.
وَأَقِيمُوا الْوَزْنَ بِالْقِسْطِ وَلَا تُخْسِرُوا الْمِيزَانَ
( 9 ) Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani.
وَالْأَرْضَ وَضَعَهَا لِلْأَنَامِ
( 10 ) Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe.
فِيهَا فَاكِهَةٌ وَالنَّخْلُ ذَاتُ الْأَكْمَامِ
( 11 ) Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba.
وَالْحَبُّ ذُو الْعَصْفِ وَالرَّيْحَانُ
( 12 ) Na nafaka zenye makapi, na rehani.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 13 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
خَلَقَ الْإِنسَانَ مِن صَلْصَالٍ كَالْفَخَّارِ
( 14 ) Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo..
وَخَلَقَ الْجَانَّ مِن مَّارِجٍ مِّن نَّارٍ
( 15 ) Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 16 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
رَبُّ الْمَشْرِقَيْنِ وَرَبُّ الْمَغْرِبَيْنِ
( 17 ) Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 18 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
مَرَجَ الْبَحْرَيْنِ يَلْتَقِيَانِ
( 19 ) Anaziendesha bahari mbili zikutane;
بَيْنَهُمَا بَرْزَخٌ لَّا يَبْغِيَانِ
( 20 ) Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 21 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
يَخْرُجُ مِنْهُمَا اللُّؤْلُؤُ وَالْمَرْجَانُ
( 22 ) Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 23 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
وَلَهُ الْجَوَارِ الْمُنشَآتُ فِي الْبَحْرِ كَالْأَعْلَامِ
( 24 ) Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwa kama vilima.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 25 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ
( 26 ) Kila kilioko juu yake kitatoweka.
وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ
( 27 ) Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 28 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
يَسْأَلُهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ كُلَّ يَوْمٍ هُوَ فِي شَأْنٍ
( 29 ) Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 30 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
سَنَفْرُغُ لَكُمْ أَيُّهَ الثَّقَلَانِ
( 31 ) Tutakuhisabuni enyi makundi mawili.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 32 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ إِنِ اسْتَطَعْتُمْ أَن تَنفُذُوا مِنْ أَقْطَارِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ فَانفُذُوا ۚ لَا تَنفُذُونَ إِلَّا بِسُلْطَانٍ
( 33 ) Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 34 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
يُرْسَلُ عَلَيْكُمَا شُوَاظٌ مِّن نَّارٍ وَنُحَاسٌ فَلَا تَنتَصِرَانِ
( 35 ) Mtapelekewa muwako wa moto na shaba; wala hamtashinda.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 36 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
فَإِذَا انشَقَّتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ وَرْدَةً كَالدِّهَانِ
( 37 ) Itakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 38 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُسْأَلُ عَن ذَنبِهِ إِنسٌ وَلَا جَانٌّ
( 39 ) Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 40 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
يُعْرَفُ الْمُجْرِمُونَ بِسِيمَاهُمْ فَيُؤْخَذُ بِالنَّوَاصِي وَالْأَقْدَامِ
( 41 ) Watajuulikana wakosefu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 42 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
هَٰذِهِ جَهَنَّمُ الَّتِي يُكَذِّبُ بِهَا الْمُجْرِمُونَ
( 43 ) Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha.
يَطُوفُونَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ حَمِيمٍ آنٍ
( 44 ) Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 45 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ جَنَّتَانِ
( 46 ) Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi atapata Bustani mbili.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 47 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
ذَوَاتَا أَفْنَانٍ
( 48 ) Bustani zenye matawi yaliyo tanda.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 49 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
فِيهِمَا عَيْنَانِ تَجْرِيَانِ
( 50 ) Ndani yake zimo chemchem mbili zinazo pita.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 51 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
فِيهِمَا مِن كُلِّ فَاكِهَةٍ زَوْجَانِ
( 52 ) Humo katika kila matunda zimo namna mbili.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 53 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ فُرُشٍ بَطَائِنُهَا مِنْ إِسْتَبْرَقٍ ۚ وَجَنَى الْجَنَّتَيْنِ دَانٍ
( 54 ) Wawe wameegemea matandiko yenye bit'ana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 55 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
فِيهِنَّ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ
( 56 ) Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa mtu kabla yao wala jini.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 57 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
كَأَنَّهُنَّ الْيَاقُوتُ وَالْمَرْجَانُ
( 58 ) Kama kwamba wao ni yakuti na marijani.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 59 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha.
هَلْ جَزَاءُ الْإِحْسَانِ إِلَّا الْإِحْسَانُ
( 60 ) Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani?
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 61 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
وَمِن دُونِهِمَا جَنَّتَانِ
( 62 ) Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 63 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
مُدْهَامَّتَانِ
( 64 ) Za kijani kibivu.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 65 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
فِيهِمَا عَيْنَانِ نَضَّاخَتَانِ
( 66 ) Na chemchem mbili zinazo furika.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 67 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
فِيهِمَا فَاكِهَةٌ وَنَخْلٌ وَرُمَّانٌ
( 68 ) Imo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 69 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
فِيهِنَّ خَيْرَاتٌ حِسَانٌ
( 70 ) Humo wamo wanawake wema wazuri.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 71 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
حُورٌ مَّقْصُورَاتٌ فِي الْخِيَامِ
( 72 ) Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 73 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ
( 74 ) Hajawagusa mtu wala jini kabla yao.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 75 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ رَفْرَفٍ خُضْرٍ وَعَبْقَرِيٍّ حِسَانٍ
( 76 ) Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
( 77 ) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
تَبَارَكَ اسْمُ رَبِّكَ ذِي الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ
( 78 ) Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.